Na Boniface Meena
WAZIRI wa Miundombinu Dk Shukuru Kawambwa, amesema serikali haisuisui kufanya upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, bali inachambua taratibu ambazo hazijakamilika.
Dk Kawambwa alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua semina ya wiki mbili inayohusu mafunzo ya usalama wa usafiri wa anga.