SERIKALI imeamua kuvisajili upya vyuo vyote vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (Veta), katika mkakati wa kuhakikisha kuwa vyuo hivyo, vinatoa elimu inayokidhi matakwa ya waajiri.
Mkurugenzi wa Veta, Kanda ya Mashariki, Sylvester Nyambo, alisema hatua hiyo inafuatia malalamiko ya muda mrefu ya baadhi ya waajiri wa wahitimu wa vyuo hivyo, kuhusu uwezo mdogo wa utendaji usiolingana na sifa zilizoko katika vyeti vyao.